Viongozi CCM DMV wakijadiliana jambo kabla ya kikao cha Faragha na Mhe.
Rais Kikwete leo Sept 19,2013 jijini Washington DC, Marekani.…
Ijumaa, 20 Septemba 2013
PHOTOS: Chris Brown & Karrueche Surrounded By Ten Bodyguards While Partying Together In L.A.
Chris Brown & Karrueche Tran are still boo'd up around L.A. together. Peep the pics of them out last night inside, plus what Chris revealed during his live TV interview with DJ Skee...
Jumatano, 18 Septemba 2013
Twanga yapania usiku wa Mwafrika Bills leo
BENDI maarufu ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ leo imepania
kuporomosha burudani ya aina yake katika onesho la ‘Usiku wa Mwafrika’
ndani ya ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam
leo.
Akizungumzia usiku wa leo, Meneja wa bendi ya Twanga Pepeta, Hassan Rehani, alisema kuwa wataendelea na amsha amsha ya kutoa shoo kali ambayo ana uhakika itawagusa wengi.
“Hivi sasa bendi yetu imedhamiria kufanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kuwahi ukumbini na kuanza kutoa burudani mapema, ili kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu wanaokuja Bilicanas na katika maonesho mengine,” alisema Rehani.
Hivi sasa Twanga Pepeta wanatamba na albamu inayokwenda kwa jina la ‘Nyumbani ni Nyumbani’ ukiwa ni utunzi wa mwanamuziki mwenye mvuto jukwaani, Kalala Hamza Kalala ‘Kalala Junior’.
Mbali ya Kalala, waimbaji wengine wanaopamba safu ya waimbaji ni pamoja na Luiza Mbutu, Haji Ramadhan ‘BSS’, Janet Isinika, Jumanne J4, Saleh Kupaza na wengineo. Kiingilio katika usiku wa leo ni sh 8,000.

Jumanne, 17 Septemba 2013
UWAKILISHI KATIKA MKUTANO MKUU TFF
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imesema uwakilishi wa ujumbe kwenye Mkutano Mkuu unaanzia
kwenye chama cha mpira wa miguu cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na
baadaye klabu ya Ligi Kuu.
Mwongozo huo juu ya uwakilishi wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu umetolewa kutokana na maombi ya Sekretarieti ya TFF kwa kamati hiyo iliyokutana jana (Septemba 16 mwaka huu) baada ya kubaini baadhi ya wajumbe wanashikilia nafasi mbili kwenye vyama tofauti.
Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba, kuna makundi ya aina tatu ya wanachama wanaounda TFF. Makundi hayo ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu.
Sekretarieti ya TFF imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kuchaguliwa wa mikoa ambao pia ni viongozi wa vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu, hivyo wana nafasi zaidi ya moja ya kuingia kwenye Mkutano Mkuu.
Hivyo, kutokana na mwongozo huo ushiriki wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu wa TFF utaanzia chama cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na baadaye klabu za Ligi Kuu.
Pia nafasi ambazo zinaweza kuwakilishwa kwenye Mkutano Mkuu kama mhusika hayupo ni za Mwenyekiti atakayewakilishwa na Makamu Mwenyekiti, na Katibu atakayewakilishwa na Katibu Msaidizi. Nafasi za ujumbe wa Mkutano Mkuu na ile ya mwakilishi wa klabu hazina uwakilishi kama mhusika hayupo.

Jumatatu, 16 Septemba 2013
Obama awasiliana na rais mpya wa Iran

Rais Obama anasema ameandikiana barua na rais mpya wa Iran, Hasan Rouhani.
Akihojiwa na televisheni ya Marekani, ABC, Obama alisema Iran inafahamu kuwa sera ya Iran ya kujaribu kuunda
silaha za nyuklia ni swala kubwa zaidi kwa Marekani kushinda silaha za
kemikali zilizotumiwa na Syria.Jumapili aliulizwa jee Iran itafikiria vipi msuko-suko wa Syria?.
Rais Obama alisema amewasiliana na rais mpya wa Iran, Bwana Rouhani.
Na alisema kuna tofauti baina ya Iran na Syria.
Alikiri kuwa mradi wa nyuklia wa Iran unavotishia Israel, ni jambo lililo karibu na masilahi ya Marekani kushinda silaha za kemikali.
Aliongeza kusema kuwa mashindano ya kumiliki silaha za nyuklia yanaweza kutibua sana eneo hilo.
Akilinganisha Iran na Syria, Rais Obama alisema anafikiri Iran inatambua kwamba kuna njia ya kusuluhisha maswala haya kidiplomasia, ingawa alikiri kuwa ni vigumu kuzungumza na Iran.
Uchaguzi wa wabunge wafanyika Rwanda

Raia wa Rwanda milioni sita leo wanapiga kura
kuwachagua wabunge katika mfumo wa vyama vingi vya kisiasa. Rwanda
inasifika sana kwa kuwa na wanamama wengi kwenye nyadhifa za uongozi wa
kitaifa.
Uchaguzi huu usio na upinzani mkubwa ni kama
kupiga muhuri tu uongozi wa chama cha RPF chake Rais Paul Kagame ambacho
kimekuwa uongozini tangu kumalizika kwa mauaji ya Kimbari mwaka 1994.Mayweather adhihirisha ubingwa wake

Floyd Mayweather ameboresha umaarufu wake kama bingwa wa masumbwi baada ya kumshinda Saul Alvarez mjini Las Vegas.
Ushindi wa Mayweather mwenye umri wa miaka 36,
umempa taji la WBC na WBA uzani wa kati. Pia ameshinda katika michuano
yote 45 aliyopigana kama mwanamasumbwi wa kulipwa.Arsenal yatembeza kichapo

Aaron Ramsey alishinda magoli 2 na kuiwezesha timu yake kuinyoa Sunderland 3-1 huku meneja Paolo Di Canio akipewa kadi nyekundu.
Goli la kwanza lilipatikana baada ya juhudi za
mchezaji mpya aliyesajiliwa na Arsenal Mesut Ozil ambaye alimwandalia
pasi murua Olivier Giroud aliyenusa nyavu.Goli hilo lilisawazishwa na Craig Gardner muda mfupi baada ya mapumziko.
Magoli mengine mawili ya Arsenal yalitiwa kimiani na Ramsey na kuiwezesha timu yake kuandikisha ushindi wa mabao 3-1 ambao ni wa tano mfululizo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)