Jumanne, 7 Januari 2014

Mazungumzo ya Diamond kuhusu kinacho endelea kati yake na Wema Sepetu na ile movie yao 2014.


Screen Shot 2014-01-06 at 10.35.29 PM
Diamond alikua kwenye Exclusive interview ya.........
XXL ya Clouds FM na kuyajibu maswali ya Raymond Mshana ambae ndio alikua anaifanya XXL kwa siku hii ya January 6, 2014.
Kwenye show ya Xmas Diamond alifanya show yake kwa ajili ya watoto Leaders Dar es salaam ambapo baadae vyombo vya habari vilimkariri akitangaza kwamba Wema Sepetu ndio mchumba wake wa sasa.
Kwenye XXL Diamond amekwepa kulijibu hilo swali ila akamzungumzia Wema na uwepo wake na kusema kua wema ni moja kati ya wasanii wakubwa na maarufu tanzania kwa upande wa burudani (celebrity) na alikua ameleta watoto na wadogo zake,
   hivyo alichofanya Diamond ni kumkaribisha Wema jukwaani awasalimie watoto kwa kuimba na kucheza pamoja sababu hata yeye ni kipenzi cha watoto.
Pamoja na hayo Diamond pia alizungumzia kuhusu movie ambayo wamecheza pamoja yeye na Wema ambayo inatarajiwa kutoka mwaka huu 2014 lakini kwa sasa bado ipo katika maandalizi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni