
Rais Obama anasema ameandikiana barua na rais mpya wa Iran, Hasan Rouhani.
Akihojiwa na televisheni ya Marekani, ABC, Obama alisema Iran inafahamu kuwa sera ya Iran ya kujaribu kuunda
silaha za nyuklia ni swala kubwa zaidi kwa Marekani kushinda silaha za
kemikali zilizotumiwa na Syria.Jumapili aliulizwa jee Iran itafikiria vipi msuko-suko wa Syria?.
Rais Obama alisema amewasiliana na rais mpya wa Iran, Bwana Rouhani.
Na alisema kuna tofauti baina ya Iran na Syria.
Alikiri kuwa mradi wa nyuklia wa Iran unavotishia Israel, ni jambo lililo karibu na masilahi ya Marekani kushinda silaha za kemikali.
Aliongeza kusema kuwa mashindano ya kumiliki silaha za nyuklia yanaweza kutibua sana eneo hilo.
Akilinganisha Iran na Syria, Rais Obama alisema anafikiri Iran inatambua kwamba kuna njia ya kusuluhisha maswala haya kidiplomasia, ingawa alikiri kuwa ni vigumu kuzungumza na Iran.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni