BENDI maarufu ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ leo imepania
kuporomosha burudani ya aina yake katika onesho la ‘Usiku wa Mwafrika’
ndani ya ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam
leo.
Akizungumzia usiku wa leo, Meneja wa bendi ya Twanga Pepeta, Hassan Rehani, alisema kuwa wataendelea na amsha amsha ya kutoa shoo kali ambayo ana uhakika itawagusa wengi.
“Hivi sasa bendi yetu imedhamiria kufanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kuwahi ukumbini na kuanza kutoa burudani mapema, ili kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu wanaokuja Bilicanas na katika maonesho mengine,” alisema Rehani.
Hivi sasa Twanga Pepeta wanatamba na albamu inayokwenda kwa jina la ‘Nyumbani ni Nyumbani’ ukiwa ni utunzi wa mwanamuziki mwenye mvuto jukwaani, Kalala Hamza Kalala ‘Kalala Junior’.
Mbali ya Kalala, waimbaji wengine wanaopamba safu ya waimbaji ni pamoja na Luiza Mbutu, Haji Ramadhan ‘BSS’, Janet Isinika, Jumanne J4, Saleh Kupaza na wengineo. Kiingilio katika usiku wa leo ni sh 8,000.