Mwanafunzi wa kike,13, (jina
linahifadhiwa) anayesoma darasa la tano katika shule ya Msingi
Unyakumi, mkoani Singida, amefanyiwa unyama kwa kubakwa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Mapunda ambaye ni dereva wa bodaboda.
Unyakumi, mkoani Singida, amefanyiwa unyama kwa kubakwa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Mapunda ambaye ni dereva wa bodaboda.
Akizungumza kwa shida kutokana na
maumivu makali aliyonayo akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
denti huyo alisema kwamba mkasa huo ulimpata Novemba 19, mwaka huu
wakati akitoka shule akielekea nyumbami kwao.
Akisimulia mkasa huo mwanafunzi huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi ni mtoto yatima wa kufiwa na baba,
mama naye aliachana na baba nikiwa na umri mdogo, nimekulia katika
shida tena kwa kulelewa na watu tofautitofauti, niliona
kitakachonikomboa ni elimu lakini ndoto yangu sasa imekufa.
“Imekufa kwa kuwa nateseka kitandani
kwa muda mrefu sasa kutokana na maumivu yaliyotokana na kubakwa.Nimekua
wa kujisaidia kitandani, nawakumbuka wazazi wangu, leo hii wangekuwepo
wangekua watetezi wagu, sina uhakika kama nitapona na kwenda shule tena.
“Kutoka shuleni hadi nyumbani ni
mwendo wa saa moja, siku hiyo niliyobakwa ilikua Ijumaa, nilikua natoka
shule nikielekea nyumbani, njiani kuna vichaka na mashamba ya mikorosho,
nilipofika karibu na banda bovu nilimkuta kijana amekaa juu ya jiwe.
“Nilijisikia vizuri sana
nilipomuona, uoga ulinitoka juu ya wanyama wakali, sikua na hofu ya aina
yoyote kama angenigeuka, nilipomkaribia alinikamata kwa nguvu,
alinivuta akanipeleka katika banda bovu.
“Nilijaribu kujinasua lakini
nilishindwa kwani alikua na nguvu kuliko mimi, niliamua kupiga kelele
ili nipate msaada toka kwa mtu yeyote anayepita, hata hivyo, hakuna
aliyejitokeza, alinifunika mdomo, alinipiga, niliishiwa nguvu,
akaniingilia, alipomaliza haja yake, akakimbilia pasipojulikana.
“Nilitokwa damu nyingi zilizotoka
sehemu za siri, niliinuka na kutembea kwa shida kwani hata kiuno kilikua
kikiuma sana, nilifika nyumbani, sikumkuta dada kwani alikuwa ana
kawaida ya kurudi usiku akitokea kazini kwake.
“Aliporudi alikuta nimeshafua nguo
zangu na nimeshalala, niliona aibu kumweleza, ilipofika Jumapili maumivu
ya kiuno na sehemu za siri yakaongezeka, nilikua nikitembea kwa shida,
ilimbidi dada aniulize nina nini? Awali niliogopa kumweleza lakini
baadaye nilimsimulia kila kitu kwani maumivu yalizidi.
“Nilishindwa hata kwenda shule,
nilipelekwa hosptali ya wilaya lakini hali yangu ilizidi kuwa mbaya.
Nikahamishiwa hospitali ya mkoa, Singida lakini sikuweza kupata nafuu,
nikaletwa hapa Muhimbili kwa gari la wagonjwa ‘ambulance’ kwani nilishindwa kukaa kwenye kiti cha basi.
“Bado sijaweza kukaa wala kuinuka,
hata kulala kwangu ni kifudifudi, nalishwa, naogeshwa kitandani, kwa
kweli sina raha hata kidogo tangu nifanyiwe unyama huo maana sijaenda
shule, wenzangu wamefanya mitihani mie sipo, nauguza mamivu.
“Nimeoza sehemu za siri hadi
makalio, natokwa na usaha, siamini kama nitapona na kwenda shule tena.
Aliyenitenda haya tunaishi naye mtaa mmoja na hajawahi kunitongoza ila
aliamua kunibaka.
“Nimefikishwa hapa Muhimbili Novemba
20, mwaka huu, naomba taarifa hizi zimfikie mama popote alipo kwani
aliachana na baba akarudi kwao Musoma,”alieleza kwa uchungu denti huyo.
Dada wa mtoto huyo anayeishi naye
aliyejitambua kwa jina moja la Rose alipoulizwa juu ya madai hayo
alikiri kutokea na ameiomba serikali imkamate mtuhumiwa ili haki
itendeke.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni