Rafiki wa karibu wa Jackie Cliff asimuliwa jinsi mrembo huyo alivyokamatwa na madawa ya kulevya China..

Rafiki wa karibu wa Jackie Cliff, Chief Rocka amethibitisha taarifa zilisosambaa kuwa msichana
aliyekamatwa na kilo 1.1 ya madawa ya kulevya aina ya Heroin huko Macau, China ni yeye.
“Amekamatwa kweli,” Chief amesema Chief.
“Nilivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand baada ya kutoka Thailand akaenda Macau, Macau ndio akakamatwa.
“Nilivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand baada ya kutoka Thailand akaenda Macau, Macau ndio akakamatwa.
“Mimi nilijua sababu nilipigia simu watu wa ubalozini baada ya kupata taarifa tu mara
ya kwanza nikawapigia watu wa ubalozi nikawaambia ‘bana, ndugu yetu
amekamatwa sasa nataka kujua process ikoje kama kuna kumuona au kama
kuna chochote.
“Kuna ubalozi mwingine mdogo upo Hong Kong
wao ndio wakaniambia mambo yalivyo kwamba alikuwa yupo yeye na watu
wengine wawili, Mtanzania na Mnaijeria, yeye ndo kakamatwa, hawa wengine
baada ya kuona wanataka kukamatwa wakakimbia,” Chief ameeleza.
Amesema kwakuwa Jackie amekamatwa
Macau ambako kuna sheria tofauti na upande wa bara wa China, adhabu yake
inaweza kuwa ndogo kuliko ile ya kunyongwa ambayo hutolewa bara.
“Inategemea ukikamatwa mainland China halafu labda ukakamatwa Macau au kwa Macau na Hong Kong ni kama uko kwetu nikama Tanzania na Zanzibar.
“Kwahiyo yeye alikokamatiwa ni kama yupo Zanzibar ni ndani ya China lakini inajitegemea lakini sheria zake sio kali sana.
”Lakini sasa mpaka wajaji kutokana
na mzigo walioubeba, wengine wanasema miaka mitatu, wengine minne,
wengine wanasema wanatoa kama Hong Kong miaka nane, so inategemea na
akiisaidia polisi akisema watu aliokuwa akiwapelekea mzigo waliko na
wakapatikana, I don’t know.”
Hata hivyo Chief amesema ameshangaa kuona jinsi Watanzania wanavyomhukumu mtu kabla ya kujua ukweli wa mambo.
“Yaani hii imereveal jinsi ambavyo
Watanzania tuko. Sio kwamba nafahamiana sana na Jackie, nimefahamiana
naye mara ya kwanza na ya mwisho, sikukaa naye hata kwa wiki tatu, I
wouldn’t end up judging someone like how people wanavyojudge kwenye
Instagram na mitandao mingine kwamba ‘kapatikana, kaumbuka, bado Jux
zamu yake, sijui nini.”
Amesema kuonana na Jackie kwa sasa sio rahisi kwakuwa wengine wanasema uwezekano huo unaweza kupatikana mwezi wa tatu mwakani.
Chief ameongeza kuwa hakuna sehemu mbaya na hatari kukamatwa na madawa ya kulevya kama China.
“Navyosema kwamba I feel sorry for
her ni kwasababu mimi nimekuwa hapa miaka mitano at least naongea
kichina yaani hata wakikifunga you can socialise with people lakini sasa
kwa yeye ambaye haiongei,… yaani ukiweka ubinadamu, ukiachana na hayo
mambo sijui ya madawa ya kulevya yule ni msichana ni kama wasichana
wengine wowote , yaani kama dada yako au demu wako akikamatwa awekwe
ndani kwenye nchi ya ugeni ni jambo kubwa yaani especially kwa mtu
ambaye umeshamfahamu kidogo huwezi kuanza kumjudge kisa amepost picha ya
Benz yake, yaani she is a hardworking woman. Suala la madawa sio zuri lakini sio kila mtu anaweza akafanya.”
Rapper huyo amesema picha zilisombaa mtandaoni zikimuonesha msichana mwenye koti la njano akiwa amekamatwa ni za Jackie.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni