Ijumaa, 3 Januari 2014

Snura amshukuru Wema kwa kuwa mtu wa mwanzo kumsaidia wakati anaanza muziki

Karibia kila msanii ambaye amefanikiwa kwa namna yoyote huwa kuna mtu aliyechangia kufika hapo alipo, upande wa Snura amemtaja mrembo Wema Sepetu kuwa ndiye aliyefungua milango ya kuelekea kwenye mafanikio ya muziki aliyonayo sasa.
snura2

Kwa mujibu wa Global Publishers, msanii wa filamu na muziki Snura Mushi amesema kuwa Wema ndiye aliyemlipia gharama za studio za kurekodi wimbo wake wa kwanza ‘Shogaake Mama’, hivyo amemshukuru kwa kuwa mchango mkubwa katika muziki wake.
wema in blue
“Namshukuru Wema, kwani alihusika sana kwenye wimbo wangu wa kwanza wa ‘Shogaake Mama’ kwani fedha yake ndiyo ilitumika kurekodi wimbo huo pia aliingiza sauti yake kwenye wimbo huo, alinibunia vazi la shoo yangu ya kwanza ambalo ninaliendeleza mpaka sasa,” alisema Snura.
Snura alifanikiwa kuingia katika chart mbalimbali za muziki Tanzania mwaka huu kwa single yake ‘Majanga’ iliyopata mafanikio makubwa yaliyomuwezesha kupata show nyingi. Single hiyo ilifuatiwa na single nyingine ‘Nimevurugwa’ ambayo hata hivyo haijafanikiwa kufikia mafanikio ya ‘Majanga’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni